Support UM News on World Press Freedom Day: Give to help sustain and expand the storytelling capacity of UM News. Your donation today will transform information into inspiration and ensure we can continue sharing stories of God’s work in the world through The UMC. Help us reach our $10,000 goal and keep this vital ministry fair, faithful, trusted and free for all!

Resumé ya 30 Avril: Interdictions ya wa LGBTQ imeondolewa, communion na Église Épiscopale imechikwa

Katika siku ya pili ya Conférence Générale, wajumbe walitumika kwa haraka  kupitia calendrier ya consentement.

Kwa sababu calendrier ya consentement iko na vitu vingi via ku voter saa mmoja, wakati ingine ni vigumu kufuatilia kile ambacho kilikubaliwa. Hata hivyo, révérend Gary Graves, secrétaire wa Conférence Générale, alisimamisha plénière ya asubuhi juu ya kuangaza décision mkuu wajumbe walikubali: kuingia katika communion na Kanisa Épiscopale.

Interdictions ya wa LGBTQ yanondolewa polepole

Wajumbe Jay Williams (gauche), Conférence ya New England, na Allie Scott, Conférence ya Wisconsin, wakiangalia agenda ya siku kabla ya kuanza plénière ya Conférence Générale ya Église Méthodiste Unie mu 30 avril huko Charlotte, Caroline du Nord. Picha na Larry McCormack, UM News.
Wajumbe Jay Williams (gauche), Conférence ya New England, na Allie Scott, Conférence ya Wisconsin, wakiangalia agenda ya siku kabla ya kuanza plénière ya Conférence Générale ya Église Méthodiste Unie mu 30 avril huko Charlotte, Caroline du Nord. Picha na Larry McCormack, UM News.

Conférence Générale inafanya mabadiliko ya kihistoria kimya kwa sera ya watu wa LGBTQ wa Église Méthodiste Unie.

Bila débat, wajumbe walichagua 667-54 kwa mabadiliko ya ihi siku hiyo ambayo inasainaruhusu assemblée législative kukubali sheria wingi . Ili kuwekwa kwenye calendrier ya consentement, maombi lazima yapokee zaidi votes 10 za "hapana" katika commission legislative na ayipashwe kubadilisha budget ya Kanisa ao dénomination.

Vitu vilivyopitishwa wakati ya asubuhi ya 30 avril kinaondoa kando ya  Plan Traditionnel uliopitishwa kwa vote ya 438-384 katika Conférence Générale la 2019. Iyi plan iliweka sheria wengi juu ya wa LGBTQ na wa clergé “wale wanaojitambulisha kuwa homosexuels”

Communion na Kanisa Épiscopale inakaribia zaidi

Communion na Kanisa Épiscopale kukubaliwa kwa wajumbe kupitia calendrier ya consentement wakati wa session ya asubuhi. Session ya Conférence Générale kilikatizwa kwa muda ili kutambua kupitishwa kwake.

Tangazo hili linakuja wakati wa “journée œcuménique” ya Conférence Générale, kuanza na ibada ya asubuhi kwa mahubiri ya Rev. Jerry Pillay, mchungaji wa kutoka Afrique du Sud katika Uniting Presbyterian Church, akaleta habari la makubaliano ya ushirika na Kanisa la Morave ilipitishwa mu 29 avril.

Kama Kanisa Épiscopale inakubali hayo, ambayo yasifanyike hadi mikutano iliyopangwa kufanyika mwaka 2027, itamaanisha kwamba hayo dénominations mawili yanatambuana kuwa ni “kanisa moja, takatifu, catholique na apostolique ambalo Injili inahubiriwa na kufundishwa kwa njia inafaayo.”

Mabadiliko ya Principes Sociaux zinapita

Église Méthodiste Unie imekubali seti mupya ya Principes Sociaux.

Wakati wa séance plénière ya asubuhi, wajumbe walichagua kupitiya calendrier ya consentement kwa votes 667-54 sehemu tatu ya Principes Sociaux zilizorekebishwa. Hizi ni pamaja na préambule mupya na sehemu mupya kuhusu Communauté ya viumbe vyote na Communauté économique. Wajumbe wanarekebisha aya ya 160 na 163 katika Kitabu cha Nidhamu (Livre de Discipline).

Wakati wa kuomboleza unyanyasaji

Watu wanaweka bougie mbele ya misalaba wakati wa Ibada ya Maombolezo, Kuungama na Matumaini mu 29 avril kwenye Conférence Générale ya Église Méthodiste Unie huko Charlotte, Caroline du Nord. Ibada hiyo iliwakumbuka wale waliotesweka na abus sexuel mu Kanisa na iliita Kanisa kubeba responsabilité. Picha na Paul Jeffrey, UM News.
Watu wanaweka bougie mbele ya misalaba wakati wa Ibada ya Maombolezo, Kuungama na Matumaini mu 29 avril kwenye Conférence Générale ya Église Méthodiste Unie huko Charlotte, Caroline du Nord. Ibada hiyo iliwakumbuka wale waliotesweka na abus sexuel mu Kanisa na iliita Kanisa kubeba responsabilité. Picha na Paul Jeffrey, UM News.

Baada kazi ya Conférence Générale ilimaliza mu 29 avril, wajumbe, wa officiers wa kanisa na waangalizi walipatana inje ya salle ya Charlotte Convention Center kuomboleza uharibifu uliofanywa na wanyanyasaji wa wanaohusishwa na kanisa.

Katika kikao cha asubuhi cha 30 Avril, wajumbe walipitisha kupitia calendrier ya consentement ombi la msamaha kutoka ku Conférence Générale kwa waathiriwa na waathirika wa tabia mbaya ya kingono katika Kanisa la Méthodiste Unie. Résolution hilo pia linahimiza na kuunga mkono kuripotiwa kwa makosa ya ngono, na linasema matumizi mabaya ya madaraka katika nafasi ya uongozi hayatavumiliwa.

Wajumbe walifurahiwa succès na maendeleo wa Africa University

Maaskofu Askofu Mande Muyombo (gauche) wa Conférence ya Nord Katanga na Gaspar João Domingos wa Conférence ya Angola wanabariki Sainte Cène wakati wa ibada ya ufunguzi wa 23 avril katika Conférence Générale ya Église Méthodiste Unie huko Charlotte, Caroline du Nord. Picha na Mike DuBose, UM News.
Maaskofu Askofu Mande Muyombo (gauche) wa Conférence ya Nord Katanga na Gaspar João Domingos wa Conférence ya Angola wanabariki Sainte Cène wakati wa ibada ya ufunguzi wa 23 avril katika Conférence Générale ya Église Méthodiste Unie huko Charlotte, Caroline du Nord. Picha na Mike DuBose, UM News.

Wajumbe wa Conférence Générale, viongozi wa makanisa na wanafunzi wa zamani walisherehekea matokeo ya Africa Univeristy na usaidizi kutoka kwa Wamethodisti Unie kotekote ambao wamesaidia kutoa elimu bora kwa wanafunzi wengi.

Kweli kwa musemeyo yake, " Hapa ndipo ambapo viongozi hutengenezwa," karibu ya 200 waliopokea diplômes zao kutoka Africa University walisimama katika salle kama James H. Salley, rais/directeur general wa Africa University Inc. vice-chancelier associé chargé chansela mshiriki kwa ajili ya maendeleo ya Africa University. Kati ya wanafunzi wa zamani hao ni wajumbe, waangalizi na watu wa kujitolea katika mkutano huo.

Hata hivyo, kufuatia débat mkali wakati wa kikao cha asubuhi cha 30 avril, plénière hilo lilikataa kuendeleza résolution ambalo lingetenga 10 millions kwa Africa University kwa muda wa miaka minne.

Katika habari nyingine

  • Wa diplômés wa Africa University wanafanya kazi katika Conférence Générale. Kulingana na tradition, wana huchukua kazi ya uongozi kama wajumbe, watafsiri na wakalimani katika mkusanyiko huu wa kimataifa.
  • Wakati wa kipindi cha asubuhi, Askofu Christian Alsted wa Région Épiscopale Nordique/Balte alitoa wito wa maombi kwa ajili ya maelfu ya watu waliouawa na vita huko Ukraine, Gaza na Est ya Congo.

Hii ni mara ya kwanza conflit armé ku Est ya Congo kutajwa katika Conférence Générale.

Est ya RD Congo imekuwa ikikumbwa na vita kwa miaka nyingi, na kusababisha mateso makubwa ya binadamu na kucheleweshwa kwa maendeleo ya inchi.

Jéthro Muyombi, mjumbe mlei kutoka Région Episcopale ya Sud-Congo, alikuwa ametoa motion mu 29 avril akiomba Conférence Générale kuombea Est ya Congo.

Révérende Esther Furaha wa Conférence Annuelle ya Kivu, mahali palipokumbwa na vita, alisema ni faraja kushuhudia maombi kwa ajili ya nchi yake.

"Maombi hayo yaliniletea hali ya utulivu na shukrani kuona communauté ya kimataifa na kanisa langu likihamasishwa kwa ajili ya nchi yangu," alisema. "Nilijisikia faraja kutokana na maneno ya huruma na matumaini yaliyotolewa wakati wa maombi." 

Butler ni producteur/editeur wa UM News.Unaweza kumpata kwa [email protected] ao 615-742-5470. Wafanyakazi kutoka UM News na United Women in Faith walichangia ripoti hii.

Kusoma habari ingine za Église Méthodiste Unie, udiandikishe ku Daily ao Weekly Digests.

Sign up for our newsletter!

Subscribe Now
Delegates, visitors and staff of the United Methodist General Conference in Charlotte, N.C., dance in the aisles following morning worship on the final day of the conference. Photo by Mike DuBose, UM News.

Synthèse wa 3 Mai: Mkutano wa kihistoria inaisha

Katika siku ya mwisho ya Conférence Générale, wajumbe waligeukia kuweka budget ambayo ita financer ministères za Kanisa kwa miaka minne ijayo — budget ambayo inapunguzwa kwa environ 40% kutoka ile iliyopitishwa mwaka wa 2016.
Askofu David Graves (droite) akitazama matokeo ya vote ya Conférence Générale mu 2 Mai ili kuidhinisha aya katika Principes Sociaux zilizorekebishwa ambazo hubadilisha msimamo wa kanisa kuhusu ndoa. Picha na Paul Jeffrey, UM News.

Synthèse wa 2 Mai: Wajumbe wanatangaza kwamba homosexualité aina tena 'incompatible”

Baraza kuu la sheria la kanisa lilipiga vote mu 2 Mai kuondoa msimamo wa dénomination unaotangaza homosexualité kuwa "incompatible na mafundisho ya Kikristo" - lugha ambayo imekuwa tangu 1972.
Mark Miller (droite) anabeba picha ya groupe inje ya Conférence Générale la Kanisa Méthodiste Unie huko Charlotte, Caroline du Nord, pamoja na watu wana wana furaha kuondolewa kwa interdiction ya ordination ya wa clergés homosexuels — katazo ambalo limeanza tangu 1984. Katikati ni Askofu Karen Oliveto, askofu wa kwanza wa Kanisa hilo ambaye ni askofu homosexuel. Muke wake, Robin Ridenour, yuko ku gauche. Picha na Mike DuBose, UM News.

Resumé ya 1er Mai: Kuondolewa kwa Interdiction ya wa clergé homosexuels, mwisho ya njia ya désaffiliation

Sujet munene ya dispute ya nguvu ku Conférence Générale katika miaka 40 iliondolewa bila débat: interdiction ya ordination ya wa clergé wale wanaojitambulisha kuwa homosexuels.

United Methodist Communications is an agency of The United Methodist Church

©2025 United Methodist Communications. All Rights Reserved